Sasa ni rahisi kupiga picha ya mitaa mipya, maeneo maarufu ya watalii na biashara za karibu. Chagua tu kamera yako, chukua video zako zinazozunguka digrii 360 na uzipakie kwenye Studio ya Taswira ya Mtaa.
Ionyeshe hadhira ya kimataifa mtaa wako, turathi zenu za kitamaduni na biashara zilizopo karibu nawe.
Isaidie miji kufuatilia hali ya misongamano barabarani, kutathmini uharibifu wa miundombinu, kuboresha shughuli za ukarabati na kutoa usaidizi wa kurejesha hali baada ya majanga.
Boresha shughuli zako za kitalii kwa kuweka katika ramani njia za kupita na maeneo yanayoweza kufikika kwa kutumia viti vya walemavu.
Hatua 3 pekee za kuchapisha picha zako za digrii 360 duniani kote
Piga picha mitaa, njia, vivutio vya watalii na biashara kwa kutumia kamera inayooana na programu ya Taswira ya Mtaa. Iwapo mtaa wako haupo kwenye
Ramani za Google, tafuta njia zingine za kudhibiti au kuchangia data kwenye ukurasa wetu wa Washirika wa Maudhui wa Ramani za Google.
*Note that Google does not certify any operational or mechanical functions. Any specific technical or logistical issues should be addressed directly with the supplier.
Beba kamera yako unapoendesha gari, unapendesha baiskeli au kutembea
Piga picha zako za digrii 360 ukiwa kwenye mwendo huku mikono yako ikiwa kwenye usukani. Tumia gari au kamera inayopachikwa kwenye kofia unapopiga picha za mtaa wako, au pachika kamera yako kwenye kiweko kidogo chenye mguu mmoja au miguu mitatu ikiwa unapiga picha za ndani.
Pakia faili nyingi kwa wakati mmoja na ukague picha zako kabla ya upakiaji kukamilika. Fikia takwimu za picha zako za digrii 360 na upange njia zako za baadaye za kupiga picha kwa urahisi.
Pata maelezo kuhusu jinsi taasisi za umma na mashirika ya utalii yanavyotumia Taswira ya Mtaa ili kuboresha mwonekano wa sehemu zao maarufu duniani kote.
Kuwezesha jumuiya za karibu kwa kutumia teknolojia ya Taswira ya Mtaa
Mnamo 2019, kikundi cha wapiga picha kilianza kuweka Zanzibar kwenye ramani. Pata maelezo zaidi kuhusu athari za mradi kwenye utalii na uchumi wa ndani.
Magari ya kusafiri mazingira yoyote yatumika kupiga picha visiwa vya French Polynesia
Mpigapicha wa mahali husika awa mbunifu kwa kutumia vigari vya gofu, boti na farasi kupiga picha za maeneo ya French Polynesia na kuyaweka kwenye ramani hivyo kuwasaidia wahudumu wa dharura wa mahali husika kuboresha huduma zao.
Kuweka Myanmar mtandaoni na kuhifadhi turathi zake za kitamaduni
Gundua jinsi kampuni ya uzalishaji wa uhalisia pepe ilivyoanza kufanya Myanmar iwe dijitali kwa kutumia Taswira ya Mtaa ili kuhifadhi turathi za kitamaduni za nchi.
Kuweka Zimbabwe kwenye ramani kupitia magari, baiskeli na mashua
Tawanda Kanhema anaweka nchi yake kwenye ramani. Pata maelezo zaidi kuhusu jinsi alivyopiga picha za Maporomoko ya Victoria na jinsi anavyoweka hata maeneo mengi zaidi kwenye Taswira ya Mtaa.
Wajuzi wa Mitaa wanaonyesha urembo wa mazingira ya Kenya kwa ulimwengu
Wajuzi wa Mitaa na wapiga picha wataalamu waliungana ili kuweka Kenya kwenye ramani na kuonyesha ulimwengu urembo wa mazingira yake. Pata maelezo zaidi kuhusu safari yao.
Mamlaka ya Utalii ya Bamuda na Miles Partnership waliungana ili kuimarisha uwepo mtandaoni wa Bamuda, kukuza ugunduzi wa biashara za karibu na kusaidia watalii kupanga safari zao.
Ili kuangazia utamaduni wa Tonga na visiwa vingine vya Pasifiki, waanzilishi wa Grid Pacific walianzisha mpango mkubwa wa kuweka funguvisiwa lote kwenye ramani na katika Taswira ya Mtaa.
Uko tayari kuchapisha video zako zinazozunguka digrii 360?
Iwapo mtaa wako haupo kwenye Ramani za Google, tafuta njia nyingine za kudhibiti au kuchangia data kwenye ukurasa wetu wa Washirika wa Maudhui wa Ramani za Google.