Kutambuliwa kwa nchi iliyozingirwa na bara - jinsi Taswira ya Mtaa ilivyotambulisha nchi ya milki za Wabudha kwa ulimwengu.

Butani inapatikana katika milima ya Himalaya na ina njia nyingi za milima, mabonde yenye rutuba na mito mitulivu. Kwa sababu hiyo, serikali ya Butani ilishirikiana na Taswira ya Mtaa katika mpango wa miezi kumi na miwili ili kuonyesha vivutio hivi fiche, huku ikikuza utalii na maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini humo.

Baada ya kupata changamoto kadhaa za uidhinishaji na za leseni za utengenezaji wa filamu, Baraza la Utalii la Butani, kwa kushirikiana na timu ya usaidizi wa kiufundi kutoka Google Singapoo, liliweza kuzindua mradi huu mnamo Mei 2020. Taswira ya Mtaa iliwapa kamera mbili za Ricoh Theta Vs, kamera moja ya Insta360 Pro, mafunzo ya ana kwa ana na vipindi vya mara kwa mara vya utatuzi ili waweze kupiga hatua.

Kilomita 2625.86

picha zilizopigwa

2,398,285

picha zilizochapishwa

Milioni 7.4

mara za kutazamwa

Kuchora ramani ya kidijitali ya mazingira maridadi ya Butani

Kabla ya mradi wa Taswira ya Mtaa, Butani haikuwa na ujuzi wa kiufundi wala vifaa vya kuwasiliana na wageni watarajiwa, jambo lililofanya iwe vigumu kwa watalii kupanga safari. Sasa, watu wowote - wawe mahujaji wa Kibudha au wageni watarajiwa - wanaweza kugundua mtandaoni nyumba za watawa za ngome za Thimpu na vijiji asili kabisa vya Punakha.

Ingawa hii ni hatua muhimu katika mpango wa serikali wa kutambulika ulimwenguni, pia ni mafanikio katika harakati za kidijitali katika Butani za kukuza jamii inayotumia TEHAMA.

Njia inayotumika zaidi kugundua Butani

Uelekezaji mahiri wa Taswira ya Mtaa umewawezesha watalii wafike katika maeneo maarufu duniani kote na kuwapa wasafiri uhuru wa kuchagua na kusafiri. Ufikiaji wa video za digrii 360 katika wakati halisi na maonyesho ya mtandaoni ya hali halisi umewasaidia wageni kuweka matarajio yao ya safari na kugundua mambo ipasavyo.

 

Ramani ya Butani kwenye Taswira ya Mtaa ya Google imesaidia nchi hiyo na watu mahususi kote ulimwenguni. Inaweza kutumiwa na masorovea wa ardhi, biashara, mashirika ya serikali, taasisi za elimu na kadhalika ili kuboresha huduma zao.

-

Dorji Dhradhul, Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Utalii la Butani

 

Huku biashara 500 mpya zikiongezwa kwenye Taswira ya Mtaa na machapisho 4,000 kuwekwa kwenye ramani za Butani, wakazi pia wameweza kunufaika kutokana na kila kitu kuanzia taarifa za moja kwa moja kuhusu hali za barabarani na mapendekezo ya njia hadi kujulikana zaidi kwa biashara za karibu.

Wataalamu wa ramani katika Taswira ya Mtaa ya Google wakiweka kamera kwenye gari nchini Butani

Taswira bora za mtaa

Mbali na kujitambulisha ulimwenguni, mpango wa serikali wa Taswira ya Mtaa umesaidia sana katika kupanga miradi ya maendeleo. Mandhari ya kurekodi filamu ambayo hayakuwa yakijulikana katika karne nyingi yamekuwa mwanzo wa mikakati ya kuhifadhi turathi za Butani. Kupitia data ya Taswira ya Mtaa, wanaweza kutathmini hali za barabara na kuziboresha panapofaa.

Butani inagunduliwa na watalii wengi kila wakati. Ingawa tumeangazia miji ishirini pekee, zimesalia kilomita 38,394 mraba za kuangazia na kuna mipango ya kusasisha mara kwa mara ramani kwa kuweka maendeleo mapya ya miundombinu; huu ni mwanzo tu wa mpango huu wa Taswira ya Mtaa.

Taswira ya Mtaa hutambulisha maeneo madogo yasiyojulikana kwa njia kubwa. Kuonyesha vivutio fiche kupitia picha bora kunaweza kubadilisha mwelekeo wa nchi na kuchangia pakubwa katika maendeleo yake.

Shiriki Picha zako mwenyewe za Taswira ya Mtaa