Sera ya wapigapicha wanaoaminika wa Taswira ya Mtaa
Sera hizi zinatumika kwa washiriki wote wanaoaminika katika Taswira ya Mtaa ambao hukusanya picha kwa niaba ya wateja wao ili zitumikie kwenye bidhaa za Google.
Sera yetu ya wapigapicha wanaoaminika wa Taswira ya Mtaa inashughulikia sehemu nne:
- Masharti ya uwazi: maelezo unayotakiwa kushiriki na wateja wako
- Desturi zilizopigwa marufuku: mambo ambayo hupaswi kufanya ikiwa unataka kuchapisha au kudhibiti picha zinazopakiwa kwenye bidhaa za Google kwa niaba ya wateja wako
- Mwongozo wa Kuweka Chapa: matumizi yanayofaa ya vipengele vya chapa za Google
- Masharti ya ubora: jinsi unavyopaswa kupanga akaunti za matangazo za Google za wateja wako
Masharti ya uwazi
Ili wateja waweze kupata manufaa kamili ya kupakia picha kwenye bidhaa za Google, wanatakiwa kuwa na maelezo sahihi ili wafanye maamuzi yanayofaa. Kwa hivyo, tunahitaji washiriki wetu wote wa mpango wa kuaminika wawe na uwazi katika kutoa maelezo yanayoathiri maamuzi haya. Mbali na kutimiza masharti yanayoelezwa hapo chini, washiriki wa mpango wa kuaminika wanapaswa kujitahidi ili kuwapa wateja wao maelezo mengine yanayofaa wanapoomba.
Unapouza huduma zako za picha kwa watu wengine, ni muhimu kuzingatia uwazi sawa na ufahamu majukumu na haki zako kulingana na sheria za mahali ulipo, chapa na watu wengine.
Gharama na ada za huduma
Washiriki katika mpango unaoaminika hutoza ada ya usimamizi kwa huduma muhimu wanazotoa na wanunuzi wa picha wanapaswa kujua iwapo watatozwa ada hizi. Angalau, wajulishe wateja wapya kwa maandishi kabla ya kila mauzo ya kwanza na ufumbue uwepo wa ada na gharama zako kwenye ankara za wateja.
Ni muhimu hasa kwa wanunuzi wa picha walio na bajeti ndogo -- ambao huenda hawana rasilimali au ujuzi wa wanunuzi wa picha nyingi -- wajue mambo wanayoweza kutarajia wanapofanya kazi na mpigapicha anayeaminika wa Taswira ya Mtaa.
Uwakilishaji wa kweli
Ukiwa mshiriki kwenye Mpango wa wapigapicha wanaoaminika katika Taswira ya Mtaa, hupaswi kujiwakilisha kwa namna inayoashiria kuwa umeajiriwa na Google. Jitambulishe kuwa huluki huru ya biashara na uwaeleze wateja majukumu machache yanayotekelezwa na Google katika uchapishaji.
Uwajibikaji wa kibinafsi
Ingawa picha zilizochapishwa huonekana kwa kawaida kwenye Ramani za Google baada ya sekunde chache, tunaweza kuzikataa picha iwapo hazitii Sera ya Ramani kuhusu Maudhui Yanayochangiwa na Watumiaji au Sheria na Masharti ya Ramani za Google.
- Iwapo picha iliyotumwa itaondolewa kwenye Ramani za Google, ni wajibu wa mpigapicha na mmiliki wa biashara kusuluhisha tatizo hilo.
- Tunapendekeza kuwa wapigapicha warekebishe au wabadilishe picha ambazo zinakiuka sera zetu - na wahakikishe kuwa zimeidhinishwa ili zitumike kwenye Ramani za Google - vinginevyo wawarudishie wateja pesa iwapo tatizo haliwezi kusuluhishwa.
Umiliki wa picha
Tunapendekeza kuwa wakati wapigapicha na wamiliki wa biashara wanajadiliana, wawe na mkataba ulioandikwa ambao unabainisha sheria na masharti ya makubaliano, dhima na haki za umiliki wa baadaye.
- Bainisha atakayemiliki picha baada ya shughuli ya kupiga picha kukamilika. Iwapo mpigapicha atamiliki picha, hakikisha kuwa mmiliki wa biashara anafahamu anavyoweza kuzitumia bila kukiuka hakimiliki za mpigapicha. Picha sawa haipaswi kuchapishwa katika akaunti mbili (kama vile akaunti ya mpigapicha na ya mmiliki wa biashara).
Kutii sheria
Hakikisha kuwa unatii sheria zote husika wakati unawahudumia wateja. Usidanganye kuhusu ujuzi wako au ubora wa kazi unayofanya. Pia, hakikisha kuwa una bima inayofaa ili kutekeleza kazi uliyopewa.
Uonekanaji wa picha
Google itaorodhesha picha kwenye Ramani za Google bila kuzingatia makubaliano yoyote ya kikazi au kibiashara kati ya washirika wengine, yakiwemo makubaliano kati ya wamiliki wa biashara na wapigapicha. Hata kama mmiliki wa biashara amemlipa mpigapicha stadi ampigie picha, hali hii haitaathiri jinsi picha zitakavyoorodheshwa au kuonekana kwenye Ramani za Google.
Hakuna ukinzani wa masilahi
Baadhi ya mipango ya Google - hasa Wajuzi wa Mitaa - inahitaji ushiriki bila kulipwa (k.m., hutafidiwa kutokana na maudhui unayochangia). Kama unatoa huduma za kulipwa (kama vile kujitangaza kuwa mtoa huduma wa kuaminika wa Taswira ya Mtaa), ni muhimu kutojumuisha huduma hizi za kulipwa kwenye huduma zisizo za kulipwa ambazo zinadhihirisha usawa (kama vile uwezo wako wa kuchapisha ukadiriaji au maoni kama Mjuzi wa Mitaa).
Matumizi yanayofaa ya Chapa za Google
Wapigapicha au kampuni ambazo zimepata hadhi ya kuaminika ndizo tu zinaweza kutumia beji ya kuaminika na chapa ya Taswira ya Mtaa ya Ramani za Google kutangaza biashara. Kama mpigapicha anayeaminika, tunakualika uzitumie kikamilifu ili kuboresha umaarufu wako. Wataalamu wa kuaminika wanaweza kutumia beji ya kuaminika, jina linalotumika kama kitambulisho na vipengele vya chapa, ikiwa ni pamoja na Ramani za Google, Taswira ya Mtaa au nembo nyingine husika. Ifuatayo ni orodha ya mambo yanayoruhusiwa na yasiyoruhusiwa. Iwapo unaamini kuwa mtu fulani anakiuka matumizi yanayoruhusiwa ya maudhui ya chapa ya Google, unaweza kuripoti matatizo hapa. Kwa maudhui mengine yoyote ya chapa za Google, unaweza kuripoti matumizi yasiyofaa hapa.
Matumizi ya Beji ya Kuaminika
- Tumia tu beji ya kuaminika na vipengele vya chapa ikiwa wewe ni mwanachama uliyethibitishwa kwenye Mpango wa wapigapicha wanaoaminika katika Taswira ya Mtaa.
- Onyesha tu beji ya kuaminika kwenye mandharinyuma meupe yaliyo na nafasi ya kutosha, popote utakapoiweka.
- Tumia tu beji ya kuaminika pamoja na nembo na jina lako au jina la kampuni yako.
- Unaweza kutumia beji ya kuaminika na vipengele vya chapa kwenye tovuti, mawasilisho, mavazi ya biashara na nyenzo za mauzo zilizochapishwa.
- Hakikisha kuwa vipengele vinavyoangaziwa zaidi kwenye ukurasa/vazi lako si beji na vipengele vya chapa.
- Usibadilishe kipengele chochote cha Ramani za Google, Taswira ya Mtaa au beji ya kuaminika, nembo au majina yanayotumika kama vitambulisho, ikiwa ni pamoja na kuongeza picha zozote, kupanua picha au kuzitafsiri.
- Usitumie beji kwa njia ya kupotosha au isiyofaa. Kwa mfano, kutumia beji kwa njia ambayo inaonyesha kuwa Google imeidhinisha bidhaa au huduma yoyote.
Wakati wa kuuza huduma zako
- Piga picha za kitaalamu za digrii 360 kama mojawapo ya huduma zako za kibiashara.
- Usiwakilishe kwa uongo wala kuficha ukweli kuwa unashiriki katika mpango wa kuaminika unapowasiliana na biashara.
- Usijumuishe huduma zozote unazolipisha (kama vile kujitangaza kuwa mtoa huduma wa kuaminika wa Taswira ya Mtaa) na uanachama wa Mjuzi wa Mitaa.
Kuweka chapa kwenye tovuti yako
- Usitumie Google, Ramani za Google, Taswira ya Mtaa, beji ya kuaminika au chapa yoyote ya biashara ya Google - au mfano wake - katika jina la kikoa.
- Unaweza kuonyesha beji ya kuaminika kwenye tovuti yako.
Kuweka chapa kwenye gari lako
- Wakati unaonyesha picha kwenye gari, unaruhusiwa tu kutumia nembo na chapa yako.
- Usionyeshe vipengele vyovyote vya chapa za Google ikiwa ni pamoja na aikoni, beji na nembo ya Taswira ya Mtaa kwenye gari.
Kuweka chapa katika sehemu ya chini kabisa au juu kabisa ya picha za digrii 360
- Tumia nembo/jina la kampuni yako kulingana na ukubwa ulio katika sehemu ya chini kabisa/juu kabisa. Rejelea mwongozo wa sera ili upate vigezo vya miundo yoyote mahususi.
- Wakati unajumuisha chapa katika sehemu ya chini kabisa ya picha au kwenye paa la gari lako, ni lazima:
- uwe na ruhusa ya kutumia chapa hiyo.
- uonyeshe tu maudhui yanayofaa (kwa mfano, kutangaza utalii nchini) au ambayo hayamilikiwi.
- Iwapo kuna ufadhili/umiliki, ni lazima chapa inayoonyeshwa:
- isiambatane na maudhui ya chapa ya Google.
- isiambatane na lugha au picha yoyote ya matangazo (isipokuwa iwe inahusiana na eneo linaloonyeshwa).
- ijumuishe "imefadhiliwa na" au tafsiri kama hiyo.
- Usitumie beji ya kuaminikia au chapa yoyote ya Google katika sehemu ya chini kabisa/juu kabisa ya picha zako za digrii 360 (zikiwemo picha zozote zinazowekwa kwenye paa ambazo zinaweza kuonekana kwenye kamera yako).
Mbali na mwongozo huu, tafadhali hakikisha kwamba unafuata Sheria za Google kuhusu Matumizi Bora, Sheria na Masharti ya Chapa, Mwongozo wa Matumizi ya Kijiografia na mwongozo mwingine wowote wa utumiaji wa chapa za biashara za Google.
Kutangaza biashara yako kwenye Google Ads
Ukipenda, unaweza kutangaza Biashara yako kwenye Google Ads kwa kutumia maneno 'mpango wa wapigapicha wa kuaminika' kwenye matangazo yako. Tafadhali kumbuka kwamba huruhusiwi kutumia chapa ya "Taswira ya Mtaa" kivyake au chapa nyingine yoyote ya Google kwenye matangazo yako.
Kuweka Chapa katika Wasifu wa Biashara yako kwenye Google
Iwapo una Wasifu wa Biashara kwenye Google, unapaswa kutii sera za Wasifu wa Biashara kwenye Google, hasa Mwongozo wa kuwakilisha biashara yako kwenye Google.
Usitumie Google, Ramani za Google, Taswira ya Mtaa au chapa nyingine yoyote ya biashara ya Google — au mfano wake, katika jina la Wasifu wa Biashara yako kwenye Google.
Unaweza kupakia beji yako ya kuaminika kwenye maelezo yako baada ya kupewa hadhi ya mpigapicha wa kuaminika.
Kumbuka: Ikiwa hutafuata mwongozo huu, unaweza kupoteza hadhi yako katika mpango na haki ya kutumia beji ya kuaminika na vipengele vingine vya kuweka chapa.
Masharti ya Ubora wa Picha za Mtaalamu wa Kuaminika
Ubora wa picha
- MP 7.5 au kubwa zaidi (pikseli 3,840 kwa 1,920)
- Uwiano wa picha wa 2:1
- Hamna mapengo kwenye mandhari ya picha
- Hamna hitilafu kuu za uunganishaji
- Sehemu zenye mwangaza/giza ziwe zinaonekana vizuri
- Ung'aavu: hamna ukungu unaotokana na mwendo, ziwe zimelengwa vizuri
- Hamna madoido au vichujio vinavyokatiza, ikiwa ni pamoja na kwenye sehemu ya chini kabisa ya picha
Muunganisho
- Picha zote za 360 zilizounganishwa ni sharti zidumishe mstari dhahiri wa mwonekano
- Piga picha katika umbali wa mita moja ukiwa ndani ya chumba na kila mita tatu ukiwa nje
- Ongeza uwezekano wa picha zako kutumika kwa kupanua mkusanyiko wako kujumuisha picha za mtaa
Ufaafu
- Ruhusa ya kuonyesha watu na mahali
- Kuweka katika eneo sahihi la kijiografia
- Hakuna sehemu zinazozalishwa na kompyuta au madoido maalum, ikiwa ni pamoja na picha inayoakisi au kupinda
- Hamna maelezo yanayozidi sehemu ya chini kabisa
- Hamna maudhui ya chuki au yanayokiuka sheria
Desturi zilizopigwa marufuku
Maudhui yasiyofaa
Maudhui Yaliyopigwa Marufuku na Kuzuiwa yanaweza kupatikana kwenye Sera ya Ramani kuhusu Maudhui Yanayochangiwa na Watumiaji.
Unaweza kuripoti maudhui yasiyofaa kwa kutumia kiungo cha "Ripoti tatizo".
Madai ya uwongo, yanayopotosha au yasiyowezekana
Tunataka wateja wa wapigapicha wanaoaminika wa Taswira ya Mtaa wafanye maamuzi yanayofaa kuhusu kushirikiana na wapigapicha wanaoaminika wa Taswira ya Mtaa, jambo ambalo linamaanisha kwamba unapaswa kuwa na uwazi na ukweli wakati unatoa maelezo kuhusu kampuni yako, huduma zako na gharama zinazohusishwa na huduma hizo na matokeo ambayo wateja wako wanaweza kutarajia. Usitoe madai ya uwongo, yanayopotosha au yasiyowezekana.
Mifano:
- kutoa madai ya uwongo ya kuhusiana na Google
- kuhakikishia nafasi ya juu kwenye Taswira ya Mtaa ya Google au Ramani za Google
Matendo ya kutoaminika, matumizi mabaya au unyanyasaji
Wateja wa Taswira ya Mtaa wanapaswa kupata huduma bora zaidi kutoka kwa mpigapicha wa Taswira ya Mtaa jinsi ambavyo wangepata ikiwa wangefanya kazi moja kwa moja na Google. Usitumie mbinu za kutoaminika, matumizi mabaya au unyanyasaji kwa wateja waliopo au watarajiwa.
Mifano:
- kusumbua wateja watarajiwa kwa kuwapigia simu nyingi
- kuweka shinikizo lisilofaa kwa mtangazaji ili ajisajili au asiondoke kwenye shirika lako
- kuruhusu wengine kufanya mitihani ya kuthibitishwa na Google kwa niaba yako
- wizi wa data binafsi
- kutoa vocha za Google Ads ili kupata malipo
Kuhusu sera zetu
Ni muhimu ufahamu na uendelee kupata taarifa kuhusu sera ya Google ya mpigapicha anayeaminika wa Taswira ya Mtaa. Iwapo tunaamini kuwa umekiuka sera zetu, tunaweza kuwasiliana nawe ili kufanya ukaguzi wa kina wa desturi zako na kukuomba uchukue hatua ya kurekebisha. Katika hali za ukiukaji uliokithiri au wa kujirudia, tunaweza kukuondoa kwenye mpango wa wataalamu wa kuaminika na tunaweza kuwasiliana na wateja wako na kuwajulisha ipasavyo. Pia tunaweza kukuzuia usichangie kwenye bidhaa za Ramani za Google.
Sera hizi ni pamoja na sheria zozote zilizopo ambazo zinaweza kutumika kwa washirika wengine, zikiwemo hizi:
Hatua zinazochukuliwa ukikiuka sera
Ukaguzi wa utii wa sera: Wakati wowote, tunaweza kukagua biashara yako ili kubaini iwapo inatii sera za mpigapicha anayeaminika wa Taswira ya Mtaa. Ikiwa tutawasiliana nawe ili kuomba maelezo kuhusiana na utii wa sera, unatakiwa kujibu kwa wakati unaofaa na uchukue hatua yoyote ya kurekebisha kwa haraka ili utii sera zetu. Tunaweza pia kuwasiliana na wateja wako ili kubaini iwapo unatii sera.
Arifa ya kutotii sera: Iwapo tunaamini kuwa unakiuka sera ya mpigapicha anayeaminika wa Taswira ya Mtaa, kwa kawaida tutawasiliana nawe ili kuomba uchukue hatua ya kurekebisha. Ikiwa hutatekeleza marekebisho tuliyoomba ufanye ndani ya kipindi husika, tunaweza kuchukua kitendo cha utekelezaji. Katika hali za ukiukaji uliokithiri au wa kujirudia, tunaweza kuchukua hatua papo hapo bila kukuarifu.
Kusimamisha mpango wa washirika wengine: Hatua yako ya kushiriki katika mipango ya Google ya washirika wengine, kama vile mpigapicha anayeaminika wa Taswira ya Mtaa ya Google, inategemea iwapo utatii sera ya mpigapicha anayeaminika wa Taswira ya Mtaa na inaweza kudhibitiwa au kusimamishwa iwapo tutabaini kuwa unakiuka sera zetu au iwapo utashindwa kushiriki katika juhudi zetu za kukagua biashara yako ili kubaini utiifu.
Kusimamishwa kwa akaunti ya Ramani: Tunaweza kusimamisha akaunti zako za Ramani za Google ikiwa utakiuka sera kwa kiwango kikubwa. Katika hali za ukiukaji uliokithiri au unaojirudia, akaunti zako za Ramani za Google zinaweza kusimamishwa kabisa na huenda usiweze kuchangia kwenye Ramani za Google. Vilevile, tunaweza kuwasiliana na wateja wako ili kuwajulisha ipasavyo.
Kuripoti ukiukaji wa sera unaofanywa na mtu au kampuni nyingine
Je, unaona kuwa mshirika mwingine anakiuka sera hii? Tufahamishe: