Tahadhari dhidi ya matukio ya ulaghai na matumizi mabaya

Kuwa mwangalifu dhidi ya wageni au anwani kutoka kwa wanaojitambulisha kama wafanyakazi wa Google ambao hutoa aina mbalimbali za usaidizi na taarifa za picha au data za hali yoyote. Tunasisitiza kwamba kampuni zinazoshiriki hazijaidhinishwa kuzungumza kwa niaba ya Google na ni lazima zijitambulishe kama makontrakta wa nje.

Tunakushauri kwa dhati kuwa wakati wowote ambapo mtu anawasiliana nawe kwa niaba ya Google moja kwa moja, tafadhali puuza mawasiliano kama hayo, haka kama yanalenga sababu zozote kama zile zilizotajwa hapa chini:

  • Kutoa huduma au mafunzo kwa niaba ya Google, kuweka vipimo, maudhui ya kidijitali, kuripoti kuhusu mitindo ya kidijitali au mifumo mipya ya kidijitali na mitindo mipya ya biashara; ushauri wa maudhui, nk.;
  • Kutoa ahadi ambazo hazilingani na utendaji wa kawaida wa huduma za Google, kama vile kuhakikisha kupata nafasi ya juu katika programu ya Tafuta, Taswira ya Mtaa ya Google au Ramani za Google;
  • Kushinikiza mshirika anayetoa kandarasi kwa kupiga simu za utangazaji au vitisho vya kuondoa maudhui kwenye mifumo ya Google.

Ni muhimu utambue kwamba Google haiajiri wapigapicha au mawakala, lakini inatoa tu orodha ya wataalamu wa kuaminika (wataalamu walio na sifa zinazoaminika za Taswira ya Mtaa) wenye uwezo wa kutumia vipengee vya mpango wa wanaoaminika kwa madhumuni ya utangazaji. Wataalamu hawa ni sehemu ya huluki huru na majadiliano yote hufanywa bila kuhusisha wala kushirikisha Google. Ni lazima wataalamu hawa wafuate sera ya wapigapicha wanaoaminika wa Taswira ya Mtaa.

Tahadhari! Wataalamu wa kuaminika wa Taswira ya Mtaa hawawezi:

  • Kujitambulisha kama wafanyakazi wa Google wala kutoa huduma kwa niaba ya Google;
  • Kuweka chapa ya Google, kama vile nembo, beji na/au aikoni ya Taswira ya Mtaa kwenye magari yao;
  • Kuweka chapa na beji za kuaminika za Google, za Ramani za Google na za Taswira ya Mtaa, au chapa nyingine zozote za biashara ya Google au vipengee kama hivyo katika jina la kikoa;
  • Kuhakikisha kuwa vipengee vimewekwa katika nafasi ya juu kwenye Taswira ya Mtaa ya Google au Ramani za Google;
  • Kushinikiza mtangazaji ajisajii au aendelee kutumia huduma za shirika lake;
  • Kutoa kuponi za Google Ads ili kupata malipo;
  • Kuhusisha huduma inayotekelezwa katika shughuli nyingine yoyote isiyo ya kitaalamu iliyo na mapendeleo, kama vile kuchapisha ukadiriaji au maoni kama Mjuzi wa Mitaa;
  • Kutumia beji ya kuaminika ili kutoa huduma mbalimbali kwa madhumuni ya mpango huu, kama vile: kuweka vifaa vya kupima wanaotembelea duka (viashiria) au zana zingine zozote za kuweka vipimo vya utendaji wa kampeni, mafunzo ya timu kwenye vyombo vya dijitali, kuripoti kuhusu mitindo ya kidijitali au mifumo mipya ya kidijitali na mitindo mipya ya biashara; ushauri wa maudhui; miradi ya majaribio n.k.

Wataalamu kwenye mpango wa wapigapicha wanaoaminika katika Taswira ya Mtaa wanaweza:

  • Kutoza ada kwa huduma zote wanazotoa;
  • Kuonyesha chapa na nembo zao kwenye gari la kampuni yao;
  • Kutumia beji ya kuaminika kwenye Wasifu wa Biashara yao;
  • Kutumia beji ya kuaminika na vipengele vya chapa kwenye tovuti, mawasilisho, mavazi ya shirika na nyenzo za mauzo zilizochapishwa.

Unaweza kutufahamisha na kuripoti masuala yanayohusu mpigapicha wa kuaminika aliyeidhinishwa kwenye Taswira ya Mtaa kwa kujaza fomu hii.

Usalama wa watumiaji ni jambo la muhimu kwetu. Kwa sababu hiyo, tunazuia matumizi ya chapa za Google na mifumo yake. Hakuna huluki iliyoidhinishwa:

  • Kutumia chapa ya Google, kama vile aikoni, muhuri na/au nembo ya Taswira ya Mtaa kwenye magari ya kampuni;
  • Kutumia chapa za Google, Ramani za Google na Taswira ya Mtaa, sifa za mtaalamu wa kuaminika au chapa nyingine za biashara za Google au vipengee kama hivyo katika jina la kikoa;
  • Kutumia chapa za Google, Ramani za Google na Taswira ya Mtaa au chapa nyingine za biashara za Google au vipengee kama hivyo kwenye mavazi (sare, n.k.);
  • Kutumia chapa za Google, Ramani za Google na Taswira ya Mtaa au chapa nyingine yoyote ya biashara ya Google au vipengee kama hivyo, katika Wasifu wa Biashara zao kwenye Google;
  • Kutumia chapa zozote za biashara za Google au beji ya kuaminika, kwa njia ambayo inaonyesha kwamba Google imeidhinisha bidhaa au huduma mahususi.