Gundua ni lini, wapi na jinsi tunavyokusanya picha za 360
Kutana na magari yanayopendeza ya Google ya Taswira ya Mtaa na upate maelezo kuhusu jinsi tunavyokusanya picha za 360 ili kuhuisha ramani ya ulimwengu.
Vyanzo vya picha
Picha za Taswira ya Mtaa hutokana na vyanzo viwili, Google na wachangiaji wetu.
Maudhui yanayomilikiwa na Google hutaja "Taswira ya Mtaa" au "Ramani za Google." Tunafunika nyuso za watu na nambari za magari katika picha zetu kiotomatiki.
Maudhui yanayochangishwa na watumiaji huambatana na jina la akaunti unaloweza kubofya au kugusa, na wakati mwingine huwa na picha ya wasifu.
Tunakotengeneza ramani mwezi huu
Huwa tunaendesha gari na kutembea uimwenguni ili kukuletea picha zinazoboresha hali yako ya matumizi na kukusaidia kugundua ulimwengu uliokuzunguka. Ikiwa ungependa kuwapungia mkono timu yetu, angalia hapa chini ili uone ni lini tutakuwa katika eneo lililo karibu nawe.
Tarehe | Wilaya |
---|
Tarehe | Wilaya |
---|
Kutokana na sababu ambazo hatuwezi kuepuka (hali ya hewa, kufungwa kwa barabara n.k.), inawezekana kuwa magari yetu hayafanyi kazi au huenda tumefanya mabadiliko madogo. Tafadhali kumbuka pia kuwa ikiwa orodha inataja jiji mahususi, huenda tukajumuisha miji na vitongoji ambako tunaweza kufikia kwa gari.
Msafara wa magari uliojiandaa kugundua maajabu ya ulimwengu
Tumetembelea maeneo mazuri sana kwenye mabara yote saba na kuna mengi zaidi yaliyosalia. Kabla hatujaanza safari, huwa tunazingatia vigezo vingi ikiwa ni pamoja na mandhari, hali ya anga na wingi wa watu ili kutumia magari yanayofaa na kukusanya picha bora kabisa.
Gari la Taswira ya Mtaa
Trekker
Kuhuisha ramani
Tukishamaliza kukusanya picha, ni wakati wa kukuonyesha zote kwenye skrini yako. Hili ni onyesho la kuchungulia ili uone timu yetu inachofanya nyuma ya pazia.
-
Kukusanya picha
Kwanza tunahitaji kuzunguka na kupiga picha za maeneo ya kuonyesha katika Taswira ya Mtaa. Tunazingatia kwa umakinifu mambo mengi, ikiwa ni pamoja na hali ya hewa na idadi ya watu katika maeneo mbalimbali, ili kuamua ni lini na wapi tutakapokusanya picha bora iwezekanavyo.
-
Kupanga picha
Ili kulinganisha kila picha na eneo lake la jiografia kwenye ramani, tunatumia kwa pamoja maelezo kutoka kwenye vihisi vilivyo katika magari vinavyopima GPS, kasi na mwelekeo. Hii hutusaidia kuunda upya njia halisi ambayo gari lilipitia na hata kugeuza na kupanga picha upya inavyohitajika.
-
Kugeuza picha ziwe za digrii 360
Ili kuzuia mapengo katika picha za 360, kamera zinazokaribiana hupiga picha zinazoingia katika eneo la picha nyingine kwa kiwango kidogo, kisha "tunaunganisha" picha hizo pamoja kuwa picha moja ya digrii 360. Kisha, tunatumia kanuni maalum za kuchakata picha ili kupunguza "mikunjo" na kuunda mwonekano laini.
-
Kukuonyesha picha sahihi
Kasi ya jinsi leza za gari huakisi maeneo hutujulisha umbali wa jengo au kitu na hutusaidia kubuni muundo wa 3D wa dunia. Unaposogea eneo lililo mbali kwenye Taswira ya Mtaa, muundo huu hubainisha panorama bora zaidi ya kukuonyesha katika eneo hilo.