Kutoka jambo la kupendelea kufanya hadi kuwa kitu maarufu ulimwenguni, jinsi hatua ya kuweka uzuri wa Polinesia ya Ufaransa kwenye ramani ilivyoleta manufaa yasiyo na kifani kwa wakazi.
French Polynesia – fukwe za mchanga mweupe, njia za matembezi marefu zinazopanda na kushuka na Vituo vya UNESCO vya Turathi za Dunia hufanya pawe maarufu katika orodha za wanaopanga safari. Ingawa baadhi ya watu wanaendelea kutamani tu kupatembelea, Christophe Courcaud aliona fursa ya kipekee ya kurekodi mahali hapa pa kuvutia na kusaidia kuboresha utalii wa Tahiti kwa kutumia Taswira ya Mtaa.
+450
orodha za biashara
zilizowekwa
Kuchanganya biashara na raha
Kutokana na upendo wake wa Taswira ya Mtaa na visiwa maridadi vya French Polynesia, Christophe alianzisha Tahiti 360 mwaka wa 2019. Kampuni hii imebobea katika upigaji picha na kupakia picha za digrii 360 za maeneo makubwa ya nje ya French Polynesia, ikiwa ni pamoja na njia za matembezi na fuo kwenye Taswira ya Mtaa. Na ingawa lengo lake kuu ni kupiga picha na kuonyesha uzuri wa maisha ya visiwa, Christophe pia anasaidia biashara za karibu zionekane zaidi kwa kutumia maonyesho bora ya mtandaoni ya kina kwenye Taswira ya Mtaa.
Kuweka Polinesia ya Ufaransa katika Ramani
Katika wakati ambapo karibu kila kitu kinapatikana kidijitali ni vigumu kuamini kwamba picha za setilaiti pekee za French Polynesia ndizo zilizokuwa zikipatikana hadi wakati Christophe na kampuni yake ya Tahiti 360 waliwasili kisiwani. Fauka ya hayo, barabara katika visiwa kama vile Bora Bora na Tahiti hazikuwa na majina yoyote, kwa hivyo kulikuwa na changamoto ya kusafiri kwa wakazi na watalii. La muhimu zaidi, ilifanya kazi ya huduma za dharura kama vile zimamoto, wahudumu wa dharura na watekelezaji wa sheria kuwa ngumu zaidi kuliko kawaida.
Niliamini kwamba Taswira ya Mtaa ina uwezo wa kuleta manufaa mengi kwenye jamii za nchini. Uwezo wa kufahamu eneo mahususi na kujua mazingira kabla hata haujaondoka nyumbani kwako hunivutia kila wakati. Hii ilionekana kuwa muhimu sana katika French Polynesia, ambapo ilikuwa vigumu sana kutoka sehemu moja kwenda nyingine.
-
Christophe Courcaud, mwanzilishi wa Tahiti 360
Baada ya kutambua manufaa ambayo Taswira ya Mtaa inaweza kuleta kwa wakazi wa kisiwa, mamlaka za maeneo mahususi zilishirikiana na Tahiti 360 ili kuweka kwenye ramani na kuzipa majina barabara zote za Tahiti, Moorea, Bora Bora, Raiatea, Maupiti, Huahine, Fakarava na Rangiroa. Christophe alitumia magari yanayoweza kusafiri katika mandhari mbalimbali, vigari vya gofu, baiskeli za umeme, boti za mtu binafsi na hata farasi ili kurekodi kilomita 1,800 katika French Polynesia. Kutokana na mchango wa Christophe na data ya kijiografia iliyoshirikiwa na mamlaka, baadhi ya mambo mengine, sasa inawezekana kupata taarifa za moja kwa moja za hali ya barabara, mapendekezo ya njia ya haraka zaidi, na maelekezo kwa biashara za karibu, kisiwani Tahiti kwenye Ramani za Google. Hii inasaidia sana haswa kwa watoa huduma za dharura ambao wanaweza kufanya kazi kwa ufanisi zaidi katika maeneo yote ya kisiwa. Mwishowe, uwezo wa kufikia picha za Tahiti 360 kwenye Taswira ya Mtaa pia umerahisisha upangaji wa miji, matengenezo ya majengo na hali za barabara.
Kufikia Eneo la UNESCO la Turathi za Ulimwengu
Ziara bora zaidi ya Tahiti 360 ni ya Taputapuatea katika kisiwa cha Raiatea. Kituo cha Turathi za Dunia cha UNESCO kinachangia pakubwa katika kuwavutia zaidi ya wageni 300,000 kwenye French Polynesia kila mwaka. Lakini, kwa kupiga picha maridadi za digrii 360, Christophe amekifanya kionekane kwa mamilioni ya watu mtandaoni. Kazi ya Christophe iliyochapishwa ya Taswira ya Mtaa imerekodi vivutio hivi vya ulimwengu kwenye vifaa vyetu na kutuwezesha kuvigundua.
Kupiga picha kisiwa kizima si kazi rahisi, lakini Christophe alikuwa amejitolea kukabili changamoto. Ili kuhakikisha kuwa alinasa maeneo yote ya Bora Bora kwa picha za digrii 360, alisafiri kisiwani kwa gari, boti na miguu. Ilimchukua Christophe siku saba kuweka kisiwa chote kwenye ramani na kukifanya kipatikane kwa kila mtu katika Taswira ya Mtaa.
Mbali na Bora Bora, Christophe pia alipiga picha barabara zote za Papeete, mji mkuu wa Tahiti na mji wa Pirae. Uonekanaji huu ulikuwa na manufaa wakati picha za miji hii miwili ziliwekwa katika Taswira ya Mtaa.
Biashara za karibu pia zilipata fursa ya kuonekana katika Taswira ya Mtaa. Makundi makubwa ya hoteli kama vile Intercontinental, Manava na Hilton, pamoja na biashara ndogo za Malazi na Chamsha, zilifurahia fursa ya kuonyesha majengo yao kwa ulimwengu wote.
Kuongeza maeneo zaidi katika orodha ya mambo ya kutimiza
Tahiti 360 inatumai kupiga picha visiwa vyote vya French Polynesia kufikia mwisho wa mwaka, huku Maupiti, Tahaa, Visiwa vya Marquesas, Visiwa vya Gambiers na Visiwa vya Austral bado vikisalia kuangaziwa. Na ingawa bado kuna maeneo mengi ya kuangazia katika French Polynesia, Christophe tayari anafikiria kuhusu mradi wake unaofuata. Tayari amekubali kushirikiana na mamlaka za karibu za Ufaransa katika mji wake wa nyumbani ili kurekodi kilomita 400 za njia za baiskeli, bustani za maua za Amiens na treni ya utalii ya Somme Tourisme. Christophe pia atapiga picha Teahupoo, ambako kutafanyika michezo ya Olimpiki ya 2024 ya kuteleza baharini. Na kabla ya hapo, anatarajia kuongeza New Caledonia, Visiwa vya Wallis na Futuna kwenye Taswira ya Mtaa ili kusaidia kuboresha maisha ya kila siku kwa wakazi na kusaidia watu zaidi kugundua paradiso hii.
Taswira ya Mtaa ni mfumo wa kushirikiana ambapo wachangiaji wanaweza kusaidia jamii kufanikiwa, biashara kukua na kuleta maajabu ya ulimwengu karibu na watu kwa kuchapisha picha bora zaidi kwenye Ramani za Google. Zaidi ya hayo, mtu yeyote anaweza kuweka maeneo anayopendelea kwenye Taswira ya Mtaa, unachohitaji tu ni kuchukua hatua ya kwanza ya kuchangia.
Gundua zaidi