Onyesha sehemu za ndani na nje za biashara yako

Picha na maonyesho ya mtandaoni huwasaidia watu waamue kutembelea biashara. Imarisha uwepo wako mtandaoni na uonyeshe biashara yako katika hali yake bora zaidi, ndani na nje. Wajulishe wateja wako mambo ya kutarajia wanapovinjari picha za Taswira ya Mtaa kabla ya kutembelea biashara.

Aikoni ya dunia ya Taswira ya Mtaa ya Google

Zaidi ya 100

nchi na maeneo kwenye Taswira ya Mtaa

Aikoni ya watumiaji wa Taswira ya Mtaa ya Google

Zaidi ya Bilioni 1

idadi ya wanaotumia Ramani za Google kila mwezi

Aikoni ya mahali katika Taswira ya Mtaa ya Google

Zaidi ya milioni 200

idadi ya biashara na maeneo yaliyoorodheshwa kwenye Ramani za Google

Mstari wa kijani katika Taswira ya Mtaa ya Google kwenye ukurasa wa Biashara

Wajulishe watu mambo ya kutarajia kupitia picha za mwonekano wa digrii 360 za sehemu ya mbele ya duka lako

Tunga picha zako za nje za kuwaongoza wageni mahali ulipo na uwaonyeshe maelezo muhimu kama vile mahali wanapoweza kuegesha, au iwapo wanaweza kuingia kwa kutumia kiti cha magurudumu.

Picha za mwonekano wa digrii 360 za Taswira ya Mtaa ya Google za sehemu ya mbele ya duka

Fanya biashara yako itambulike kupitia onyesho la mtandaoni

Wakaribishe wateja ndani ili uwasaidie wafahamu biashara yako na huduma au bidhaa zilizomo kabla wafike. Piga picha za majengo yako, rafu za bidhaa na menyu kisha uzichapishe kwenye Taswira ya Mtaa mwenyewe, au kwa usaidizi wa mtaalamu.

Anzisha onyesho lako la mtandaoni
Onyesho la ndani la mwonekano wa digrii 360 la Wonders Boutique kwenye Taswira ya Mtaa ya Google katika Zanzibar

Wavutie wageni wako warudi kwa kuweka picha mpya

Je, umebadilisha muundo wa bidhaa au umeanza kuuza bidhaa mpya? Sasisha picha zako kwenye Taswira ya Mtaa.  Dhibiti picha zako za mtandaoni, kwa kuwafahamisha wateja wako mara kwa mara kuhusu mabadiliko na ofa za kufana.

Sehemu ya mbele ya biashara kwenye Taswira ya Mtaa ya Google kutoka kwenye Getty Images - Tinpixels
Mstari wa manjano katika Taswira ya Mtaa ya Google kwenye ukurasa wa Biashara

Jinsi ya kuanza

Aikoni ya kamera ya Taswira ya Mtaa ya Google

Tafuta kamera au umwajiri mtaalamu

Pegman ya Taswira ya Mtaa ya Google ikipiga picha

Piga picha zako

Taswira ya Mtaa ya Google - chapisha picha ukitumia Studio ya Taswira ya Mtaa

Chapisha picha zako